Baura kwa Wazazi
Sasa ni muda mgumu kwa wote duniani. Tumehuzunika sana kufunga madarasa zetu za kawaida kwa watoto. Tunajua imeumiza maisha mengi. Tunasubiri ushauri wa serikali ya mtaa, lakini tunatarajia kufungua tena haraka iwezekanavyo.
Licha changamoto, tunaendelea kusaidia jamii. Taasisi tumekumbana na changamoto nyingi tayari, hivyo tusisahau tuko pamoja. Tusipoteze mstari wa mawasiliano, viunganisho, na mahusiano. Tunawashukuru jamii kwa imani yao kwetu. Tunawaamini pia.
​
Kuna habari njema! Bila shaka, wewe mzazi, unaweza kumfundisha mtoto wako wenyewe nyumbani, hata kama huna smartphone, hata kama hujui kiingereza, hata kama haujaenda shuleni. Kama unaweza kusoma, inatosha kwa kuanza kufundisha. Wewe ni mtu mzima, menta wake wa kwanza, na umeshajifunza vitu vingi kuliko yeye katika maisha yako. Mtoto hukutazama wewe mzazi na hukuiga. Yaani, ukiposoma atasema “Naomba nisomea pia. Nijifunze nawe!” Mzazi ndiye mwalimu bora kwa mtoto, kwa sababu tayari mnapendana! Usijali, tunakusaidia hatua kwa hatua:
1. Tafuta mtandao. Kama una whatsapp, ingie kikundi chetu cha wazazi kupitia Katibu Madaam Neema. Kama huwezi kukopa smartphone au ukiwa na shida lolote, tujulishe, ile tuweze kupanga zamu yako maktabani.
2. Uje Tovuti yetu, chagua lugha yako, na piga "Kwa Wazazi". Utaona vitabu, Habari, Barua zako, wavuti wa elimu huru, na mitaala ya wanafunzi wetu.
3. Piga Mitaala. Tafuta darasa la mtoto wako.
4. Msaidie mtoto kukumilisha mazoezi daftarini/ukurasani
5. Piga "Pakia Mazoezi" (Tuma/Upload) kwa kamera ya simu
6. Jisomea mwenyewe kwa elimu yako.
​
​